Tuesday 28 July 2015

HII NDIO AJALI YA BASI LILILOGONGA TRENI NA KUUA WATANO MOROGORO

Askari wa usalama barabarani wakitazama basi hilo baada ya kugonga treni  katika eneo la Kibaoni, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu watano akiwamo dereva wa basi hilo aliyefariki wakati akipatiwa matibabu.

Askari wa usalama barabarani akiandika maelezo ya ajali ya basi hilo lililogonga treni  katika eneo la Kibaoni, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Wednesday 11 March 2015

KONTENA LAANGUKIA BASI NA KUUA ABIRIA WOTE MAFINGA

Basi hilo kampuni ya Majinja likiwa limeangukiwa na kontena na kuharibiwa vibaya katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Changarawe, wilayani Mafinga mkoani Iringa na kuhofiwa kuua abiria wote waliokuwamo humo. Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam wakati lori lililokuwa limebeba kontena hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya. 
Abiria wakiwa wamening'inia baada ya kupondwa na kontena hilo.
Baadhi ya wasamaria wakishuhudia ajali hiyo eneo la tukio tayari kwa kutoa msaada wa kunasua miili iliyonasa baada ya kupondwa na kontena.
Baadhi ya miili ikining'inia baada ya kupondwa na kontena eneo la tukio wilayani Mafinga mapema leo.

Friday 5 September 2014

HII NDIO AJALI YA MABASI ILIYOUA WATU ZAIDI YA 60 MUSOMA LEO

Tunaomba radhi kwa picha hizi, lakini hii ndio hali halisi ya ajali mbaya zaidi kutokea kwa mwaka huu ambapo maisha ya wenzetu zaidi ya 60 yalikatishwa ghafla kutokana na uzembe wa watu wachache tu wenye haraka zao ambazo hata hivyo ziliishia hapa. Tunatoa wito kwa abiria kuchukua hatua za haraka ili kuepusha hasara hii ya nguvukazi ya taifa letu. Mungu aziweke mahali pema roho za wote waliopoteza maisha katika ajali hii ya mabasi ya J4 na Mwanza Coach iliyotokea leo.
Miili ya marehemu ikiwa imelazwa chini baada ya kunasuliwa kutoka kwenye moja ya mabasi hayo.
Miili ya marehemu ikiwa bado imening'inia kwenye moja ya mabasi hayo.
Hili ndilo moja ya mabasi hayo huku miili ya marehemu ikiwa bado haijatolewa ndani yake, pamoja na dereva mmojawapo anayetajwa kuhusika kwenye uzembe huo. 

Wednesday 30 July 2014

BASI LA MOROBEST LAGONGANA NA LORI NA KUUA 17

Basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam, lenye namba za usajili T 258 AHV eneo la tukio baada ya kugongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi. 
Majeruhi wa ajali ya basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam, wakiwa wamelazwa chini kusubiria huduma ya matibabu hospitalini. Watu 17 wamethibitishwa kufariki dunia mpaka sasa katika ajali hiyo ambayo basi hilo lenye namba za usajili T 258 AHV liligongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.
Wasamaria wakihaha kunasua majeruhi kwenye basi la Morobest lililopata ajali likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam, baada ya kugongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.
Miili ya abiria wa basi la Morobest lenye namba za usajili T 258 AHV waliofariki dunia baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.

Friday 11 July 2014

KUNA USALAMA KWELI AU...?

Dereva huyu wa basi lenye abiria takribani 60 akilipita lori lenye mizigo kwenye eneo ambalo si salama katika barabara la Morogoro hivi karibuni.

MIUNDOMBINU MIBOVU

Magari na bajaji zikipita kwa tabu katika moja ya barabara za jiji la Dar es Salaam baada ya mvua kubwa kunyesha hivi karibuni. Hivi kodi tunazolipa zinakwenda wapi kama hali yenyewe ndio hii? Je, kuna umuhimu wa kulipia ushuru wa baabara?

TRAFIKI AKIWA KAZINI

Trafiki huyu wa kike akijaribu bila mafanikio kukabiliana na foleni Dar baada ya kunyesha mvua kidogo tu.